Mbarikiwa - Kale Nilitembea - Usifiwe Msalaba 22

Chorus / Description : Usifiwe Msalaba Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!
Kale nilitembea Nikilemewa dhambi
Nilikosa msaada, kuniponya mateso.

Kale Nilitembea - Usifiwe Msalaba 22 Lyrics

Kale nilitembea Nikilemewa dhambi
Nilikosa msaada, kuniponya mateso.

Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!

Hata nilipofika, Mahali pa Msalaba,
Palinifaa sana, Sitasahau kamwe.

Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!

Hicho ndicho chanzo, Cha kufurahi kwangu.
Hapo ndipo mzigo, Uliponituliwa.

Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!

Panapo msalaba, Kinatolewa cheti,
Cha kuingia Mbinguni, Kisicho cha kanisa.

Usifiwe Msalaba Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!

Yule Bwana mjinga, Likwenda bila cheti,
Kitumai kwingia, Kama walio nacho.

Usifiwe Msalaba Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!

Lipofika langoni, Akaulizwa cheti,
Cha kumwonyesha Bwana, Akakutwa hanacho.

Usifiwe Msalaba Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!

Lituhuzunishalo, Ni ninyi msio nacho,
Kuwa kama mjinga, Kwa siku ya arusi!

Usifiwe Msalaba Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!

Ubavuni mwa Yesu, Mlitokea damu,
Chemchemi ya uzima, Itakasayo roho.

Usifiwe Msalaba Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!

Jitahidi wingie, Damuni mwa Mwokozi,
Utafutiwa dhambi, Toka rohoni mwako.

Usifiwe Msalaba Lisifiwe kaburi!
Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!

Kale Nilitembea - Usifiwe Msalaba 22 Video

  • Song: Kale Nilitembea - Usifiwe Msalaba 22
  • Artist(s): Mbarikiwa


Share: