Lyrics Page

Mungu Mwaminifu

By Guardian Angel + Rozinah Mwakideu

1,324 views Jun 6, 2026 updated

Eeh Yahweh, eeh Yahweh

Wewe ni Mungu mwaminifu

Hubadiliki kamwe


Wewe sio mwanadamu

Eti useme uwongo

Au mwana wa mwanadamu

Ubadilishe mawazo


Ukisema jambo Baba, Unatenda

Oooh Yahweh, eeh

Nakuabudu, nakuinua

Kwa uaminifu wako

Kwa uaminifu wako


Ahadi zako za milele

Ooh Yahweh Yahweh Baba


Eeh Yahweh, eeh Yahweh

Wewe ni Mungu mwaminifu

Hubadiliki kamwe


Eeh Yahweh, eeh Yahweh

Wewe ni Mungu mwaminifu

Hubadiliki kamwe


Nilidhani yamekwisha

Mambo ya mziki niachane nayo

Ukanipa fursa tena

Niimbe watu wako wakuone


Nimeona wema wako

Mkono wako umeniihifadhi Baba eeh

Eeh Yahweh

Wewe ni Mungu mwaminifu


Mwisho mwisho wa mawazo yangu

Ndio mwanzo wa yako

Ninapodhani nimemaliza

Ndio wewe unaanza


Ulingoja Lazaro afe

Ndio ukatokea

Ukamuita Lazaro toka sasa


Eeh Yahweh, eeh Yahweh

Wewe ni Mungu mwaminifu

Hubadiliki kamwe


Eeh Yahweh, eeh Yahweh

Wewe ni Mungu mwaminifu

Hubadiliki kamwe


Wazazi wanaweza kuniwacha

Wewe ni Mungu mwaminifu

Watoto wanaweza kugeuka Baba

Wewe ni Mungu mwaminifu


Misingi ya dunia ikitingizika

Wewe ni Mungu mwaminifu

Ninaowapenda wakinitenga

Wewe ni Mungu mwaminifu


Eeh Yahweh, eeh Yahweh

Wewe ni Mungu mwaminifu

Hubadiliki kamwe


Eeh Yahweh, eeh Yahweh

Wewe ni Mungu mwaminifu

Hubadiliki kamwe


Eeh Yahweh, eeh Yahweh

Wewe ni Mungu mwaminifu

Hubadiliki kamwe


Eeh Yahweh, eeh Yahweh

Wewe ni Mungu mwaminifu

Hubadiliki kamwe

Official Video

Save Your Favorites

Create a free account to save songs, build your personal library, and connect with the Zion community.

Create Free Account

Join the Zion Community

Create a free account to save your favorite lyrics, submit song suggestions, and connect with fellow worshippers.

No spam. Unsubscribe anytime.