Ujulikane Lyrics

By Karwirwa Laura

Lyrics

Nisijione mkamilifu kwa nguvu yangu

Nitaweza pekee yangu

Nisiamini hekima yangu

Juhudi zangu, nikutazamie Mungu

Watakao nisikia wakinishangilia,

Niwaelekeze kwako ooh

Watakaonifuata nikikufuata, tuje kwako

Na chochote kile itaenda sawa

Sio mimi ni wewe ujulikane

Na popote pale nitaenda baba

Sio mimi ni wewe ujulikane


Ujulikane ujulikane

Ewe Yesu ujulikane

Ujulikane ujulikane

Ewe Yesu ujulikane


Kwa maneno yangu tena matendo yangu

Kama vile maji ifunikavyo bahari

Natamani wewe ujulikane

Uokoe waliofungwa,uponye waliozidiwa

Uinue waliolemewa aah

Hakuna usichokiweza Baba aah


chochote kitaenda sawa

Sio mimi ni wewe ujulikane

Na popote pale nitaenda baba

Sio mimi ni wewe ujulikane


Ujulikane ujulikane

Ewe Yesu ujulikane

Ujulikane ujulikane

Ewe Yesu ujulikane


Uokoe waliofungwa,uponye waliozidiwa

Uinue waliolemewa aah


Ujulikane ujulikane

Ewe Yesu ujulikane

Ujulikane ujulikane

Ewe Yesu ujulikane

KARWIRWA LAURA ft ALICE KIMANZI - UJULIKANE (SKIZA 9046027)

Now Playing...