Lyrics Page

Unajibu Maombi

By Upendo Kilahiro

3,933 views Jun 6, 2026 updated

Unajubu maombi Unajibu maombi
Unajibu maombi Nakuamini Bwana

Ezekia alipougua alikulilia ukamsikia
Ukamponya na kumwongezea mwaka, Maana unajibu maombi,
Nami leo nakuita Baba usinifiche uso wako
Na wale waliokata tamaa, maana wewe u mwaminifu

Unajubu maombi Unajibu maombi
Unajibu maombi Nakuamini Bwana

Umesema ikiwa watu wako Tulioitwa kwa jina lako Tutajinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wako
Na kuziacha njia zetu mbaya, utasikia toka mbinguni
Na kutusamehe maovu yetu na kuiponya nchi yetu

Unajubu maombi Unajibu maombi
Unajibu maombi Nakuamini Bwana

Nakuabudu Mungu mwaminifu, wewe ni Mungu usiyeshindwa.
Mungu unashika maagano nakuabudu Bwana
Sikio lako sio nzito, wewe ni Mungu uliyekaribu
Toka mbinguni sikia na kujibu, Nakuabudu Bwana

Unajubu maombi Unajibu maombi
Unajibu maombi Nakuamini Bwana

Unajubu maombi Unajibu maombi
Unajibu maombi Nakuamini Bwana

God Answers Prayers


Official Video

Save Your Favorites

Create a free account to save songs, build your personal library, and connect with the Zion community.

Create Free Account

Join the Zion Community

Create a free account to save your favorite lyrics, submit song suggestions, and connect with fellow worshippers.

No spam. Unsubscribe anytime.