Usifadhaike Lyrics

By Reuben Kigame

Lyrics

Usifadhaike ndugu yangu wee 

Ule nini unywe nini kila siku 

Ama uvae nini dada yangu wee 

Baba wako wa mbinguni ashugulika 

Asema u wathamani kuliko wale ndege 

wasiopanda wa kuvuna aah 

Na tena u wathamani kuliko na maua ya kondeni 


Usifadhaike mteule we 

Majaribu na maonjo kila upande 

Ukidharauliwa na kusemwa semwa eh 

Hata imani yako yadidimia 

Asema anafahamu wewe una nguvu ndogo 

Lakini umesimama 

Na tena yuko na wewe hadi mwisho wa dahari 

Kwa hivyo usifadhaike 


Usifadhaike oh mjane wee 

Uliyeishi naye amekuacha 

Na watoto wako sasa ni yatima eeh 

Marafiki na jamii wametoroka 

Asema anasikia sauti ya mjane Oh ooh amwitapo 

Na tena yeye ni Baba wa yatima wote usifadhaike 


Unalia nini ndugu yangu wee 

Kodi ya nyumba na kazi huna 

Na watoto wako hawana karo 

Hata uko shuleni wamefukuzwa 

Oh ooh ooh anasema wewe ni wa maana sana kuliko vyote 

Na tena umeandikwa kwa kiganja chake oh ooh usifadahike 


Usijaribu kufadhaika (usifadhaike) 

Yeye ana hesabu ya nywele zako (usifadhaike) 

Ukifadhaika utakonda (usifadhaike) 

Kaka yangu wee (usifadhaike) 

Yeye anajua kesho (usifadhaike) 

Usifadhaike mummy (usifadhaike) 

Mtoto usifadhaike (usifadhaike) 

Hizi ni ahadi zake (usifadhaike)


Usifadhaike by Reuben Kigame and Sifa Voices

Now Playing...