Ni tabibu wa karibu; tabibu wa ajabu;
na rehema za daima; ni dawa yake njema.
Imbeni, malaika, sifa za Yesu Bwana;
pweke limetukuka jina lake Yesu.
Hatufai kuwa hai, wala hatutumai,
ila yeye kweli ndiye atupumzishaye.
Imbeni, malaika, sifa za Yesu Bwana;
pweke limetukuka jina lake Yesu.
Dhambi pia na hatia ametuchukulia;
Twenendeni na amani hata kwake mbinguni.
Huliona tamu jina, la Yesu kristo Bwana,
yuna sifa mwenye kufa asishindwe na kufa.
Kila mume asimame, sifa zake zivume;
Wanawake na washike kusifu jina lake.
Na vijana wote tena, wampendao sana,
waje kwake wawe wake kwa utumishi wake.
Write a review/comment/correct the lyrics of Ni Tabibu Wa Karibu - Imbeni Malaika Sifa Kwa Yesu Bwana (9):