Lyrics Page

Wewe ni Baba / Nikitafakari Jinsi Mungu

By Martha Mwaipaja

4,810 views Jun 15, 2026 updated Verified editorial review

Martha Mwaipaja's song 'Wewe Ni Baba' is a Swahili worship song that reflects on God's personal love and care, especially for those who feel rejected or abandoned. The lyrics contrast human rejection with God's faithful fatherhood, declaring that God is a Father to the fatherless and a husband to the widowed. The song expresses gratitude for God's goodness and intercedes for others who are suffering, including widows, orphans, and the sick. It emphasizes that God is not like humans who abandon, but a loving Father who comforts and provides.

Lyrics Verified by Editorial Team

Nikitafakari jinsi Mungu Alivyonipenda mimi 
Nikitafakari jinsi Mungu Alivyonipenda mimi 
Hata kunithamini mimi niliyedharauliwa na watu 
Hata kunithamini mimi niliyedharauliwa na watu . .

Kweli nimejua Mungu wangu, Yeye sio mwanadamu (x2)
Kama angekuwa mwanadamu, nisingefika leo (x2) 
Maana katika kilio changu wengi walinitenga 
Maana katika machozi yangu wengi walinitenga 
Sikumwona hata mpendwa wa kunifariji 
Nikalia Mungu wangu mbona umeniacha 
Ona umeacha fedheha katika maisha yangu 
Mungu wangu akasema niko Baba mwenye upendo 
Maana mimi naitwa Baba kwa wasio na Baba 
Maana mimi ninaitwa mume kwa wasio na mume . .

Wewe ni Baba mwema kwangu, wewe ni Baba 
Wewe ni Baba mwema kwangu, wewe ni Baba 
Uhimidiwe Mungu wangu, wewe ni Baba ah
Uhimidiwe Mungu wangu, wewe ni Baba ah . .

Wewe ni Baba wa watu wote 
Naomba tazama watu wako 
Ni wengi wanalia wanakuhitaji Baba 
Ni wengi wanajuta wanakuhitaji Yesu 
Tazama wengi ni wajane 
Tazama wengi ni yatima 
Tazama wengi ni wagonjwa 
Tazama wengi wametengwa . .

Wengine uchumi umekuwa ni jangwa kwao 
Wengine utasa umekuwa fedheha kwao 
Watazame Baba aaah . .

Wewe ni Baba mwema kwangu, wewe ni Baba 
Wewe ni Baba mwema kwangu, wewe ni Baba 
Uhimidiwe Mungu wangu, wewe ni Baba ah
Uhimidiwe Mungu wangu, wewe ni Baba ah 

Official Video

Save Your Favorites

Create a free account to save songs, build your personal library, and connect with the Zion community.

Create Free Account

Join the Zion Community

Create a free account to save your favorite lyrics, submit song suggestions, and connect with fellow worshippers.

No spam. Unsubscribe anytime.