Lyrics Page
Karibu Zaidi Na Wewe Mungu Wangu
2,790 views
Jun 6, 2026 updated
Karibu zaidi, Bwana wangu
Siku zote niwe Karibu na wewe,
Karibu zaidi Mungu wangu.
Mimi nasafiri Duniani,
Pa kupumzika Sipaoni,
Nilalapo niwe Karibu na wewe,
Karibu zaidin Mungu wangu.
Na kwa nguvu zangu Nikusifu;
Mwamba, uwe maji Ya wokovu;
Mashakani niwe Karibu na wewe;
Karibu zaidi Mungu wangu.
Na nyumbani mwa juu, Baba yangu,
Zikikoma hapa Siku zangu,
Kwa furaha niwe Pamoja na wewe,
Karibu kabisa Mungu wangu.