Sitanyamaza Lyrics

By Rose Muhando

Lyrics

Matendo nitalia, Kwa sinani nitaomboleza

Sodoma nitanung’unika, Mipakani nitashambulia

Mijini wameniacha,Kila mara nitashambulia

Maisha ya wanadamu, Yamenichosha….


Oh oh mimi

Sitanyamaza, wala sitanyamaza

Lakini nitalipa ujira wa vifuani mwao

Maovu yenu ninyi, pamoja na baba zenu

nasema nitalipa ndio mjue mimi ni Bwana

Mmefukiza uvumba, na kunitukana

Kwa ajili ya haya mtajutia vitani mwenu 


mmefanya uzinzi katikati ya milima

Usiku wa manane mmefanya ukahaba

Kwenye njia kuu na vichochoro mmefanya mapatano

Kwenye mialoni na mipera mmefanya machukizo 


Ulitumaini uzuri wako ukafanya ukahaba

Kila kijana aliyepita ulimwona anafaa

Awe mzuri na sura mbaya ulifunua marinda


Wako wapi wapenzi wako? Mbona sasa unakonda?

Wako wapi mapenzi zako? Mbona sasa unakonda?



Miji mizuri imekuwa ukiwa

Majumba mazuri yamefungwa kabisa

Wana wa wana wamebaki yatima

Kiburi cha muwamu, imekoma kabisa x2


Hebu sasa piga kelele uliye kahaba,

Shika kinubi omboleza upate kukumbukwa x2


Nirudieni mimi niwasamehe, Nasema mgeukeni sasa niwaponye

Nirudieni mimi niwasamehe, Nasema mgeukeni sasa niwaponye x2


Lakini Bwana asema hivi, nitawaponya

Yeye mwenyewe aahidi, nitawabariki

Mimi ni alfa na omega, mwanzo na mwisho

Jamani mimi ni mungu, mwingine hapana


Nirudieni mimi niwasamehe, 

Nasema mgeukeni sasa niwaponye x2

Rose Muhando -Sitanyamaza

Now Playing...