Lydia Odhiambo - Nikufananishe Na Nani Bwana

Chorus / Description : Nikufananishe na nani Bwana
Nimetambua hufananishwi

Nikufananishe Na Nani Bwana Lyrics

Nikufananishe na nani Baba 
Nimetambua hufananishwi 

Uliumba mbingu kwa neno lako 
Ukaumba mji kwa neno lako 
Ulimwengu wote na vyote vilivyomo 
Vilikuwako kwa uwezo wako. 
Hapo mwanzo kulikuwako na neno 
Naye neno alikuwako kwa Mungu 
Naye neno alikuwa Mungu mwenyewe 
Nimetambua hufananishwi 

Nikufananishe na nani Bwana 
Nimetambua hufananishwi (*2) 

Umeinuliwa juu ya vyote Bwana 
Ufalme wako umetamalika 
Viumbe vyote vyakuabudu Jehovah 
Nimetambua hufananishwi 
Ndege angani wakusifu Bwana 
Samaki baharini wakuinua Jehovah 
Miti mimea zakuimbia wimbo mpya 
Nimetambua hufananishwi 

Nikufananishe na nani Bwana 
Nimetambua hufananishwi (*3) 

(Interlude) 

Nimekuona Baba ukiokoa wenye dhambi 
Ukiweka huru waliofungu 
Umewalisha wajane na watumwa 
Nimetambua hufananishwi 
Kwa jina lako mapepo hutoroka 
Kwa jina lako viwete watembea 
Kwa jina lako visiwi wasikia 
Nimetambua hufananishwi 

Nikufananishe na nani Bwana 
Nimetambua hufananishwi (*2) 

(Interlude 2) 

Nikufananishe na nani Bwana 
Nimetambua hufananishwi (*2) 

Nikufananishe Na Nani Bwana Video

  • Song: Nikufananishe Na Nani Bwana
  • Artist(s): Lydia Odhiambo


Share: