Chorus / Description :
Nikufananishe na nani Bwana
Nimetambua hufananishwi
Nikufananishe na nani Baba
Nimetambua hufananishwi
Uliumba mbingu kwa neno lako
Ukaumba mji kwa neno lako
Ulimwengu wote na vyote vilivyomo
Vilikuwako kwa uwezo wako.
Hapo mwanzo kulikuwako na neno
Naye neno alikuwako kwa Mungu
Naye neno alikuwa Mungu mwenyewe
Nimetambua hufananishwi
Nikufananishe na nani Bwana
Nimetambua hufananishwi (*2)
Umeinuliwa juu ya vyote Bwana
Ufalme wako umetamalika
Viumbe vyote vyakuabudu Jehovah
Nimetambua hufananishwi
Ndege angani wakusifu Bwana
Samaki baharini wakuinua Jehovah
Miti mimea zakuimbia wimbo mpya
Nimetambua hufananishwi
Nikufananishe na nani Bwana
Nimetambua hufananishwi (*3)
(Interlude)
Nimekuona Baba ukiokoa wenye dhambi
Ukiweka huru waliofungu
Umewalisha wajane na watumwa
Nimetambua hufananishwi
Kwa jina lako mapepo hutoroka
Kwa jina lako viwete watembea
Kwa jina lako visiwi wasikia
Nimetambua hufananishwi
Nikufananishe na nani Bwana
Nimetambua hufananishwi (*2)
(Interlude 2)
Nikufananishe na nani Bwana
Nimetambua hufananishwi (*2)