24 Elders - Baba Tunasogea

Chorus / Description : Baba tunasogea, Baba tunasogea
Chini ya miguu yako
Baba tunasogea

Baba Tunasogea Lyrics

Baba tunasogea, Baba tunasogea 
Chini ya miguu yako 
Baba tunasogea 

Baba tunasogea, Baba tunasogea 
Chini ya miguu yako 
Baba tunasogea 

Kama mwanamke aliyetokwa na damu 
Alisogea chini yako 
Akaguza vindo la vazi lako, damu ikakauka 
Nasi twasogea chini chini yako 
Sema neno moja maisha yetu yapone 

Baba tunasogea, Baba tunasogea 
Chini ya miguu yako 
Baba tunasogea 

Hakuna aliyekuja mbele zako akatoka na kilio 
Yeyote aliyekuja kwako Bwana alitoka na furaha 
Nakumbuka Hanna ekaluni alivyosogea chini yako 
Akatoka na Samweli, Ibrahimu na Isaka 
Na mimi nasogea chini yako najua hutaniacha 
mikono wazi, Nakuja mbele zako Bwana 
Sema neno moja 

Baba tunasogea, Baba tunasogea 
Chini ya miguu yako 
Baba tunasogea 

Kama Zakayo alivyopanda juu ya mti ukamwona 
Ukamwambia Zakayo shuka upesi chini yako 
Nasi twasogea chini chini yako 
Ili wokovu wako uingie nchini mwetu 
Nasi twasogea chini chini yako 
Ili furaha yako iingie manyumbani mwetu  

Baba tunasogea, Baba tunasogea 
Chini ya miguu yako 
Baba tunasogea 
...

Baba Tunasogea Video

  • Song: Baba Tunasogea
  • Artist(s): 24 Elders


Share: