Chorus / Description :
Jina la Yesu dawa, jina la Yesu ni dawa
Jina la Yesu dawa, jina la Yesu ni dawa
Eeh ni dawa, jina la Yesu ni dawa
Nasema ni dawa tosha, jina la Yesu ni dawa
Kuna watu wenye majina
Lakini walipokufa walisahauliwa
Lakini jina la Yesu ni jina la kipekee
Usisahau kuita jina la Yesu kila wakati
Jina la Yesu dawa, jina la Yesu ni dawa
Jina la Yesu dawa, jina la Yesu ni dawa
Eeh ni dawa, jina la Yesu ni dawa
Nasema ni dawa tosha, jina la Yesu ni dawa
Wacha niseme Mungu kauliza kwenye kiti cha enzi
Kikao kilipokaa kule Mbinguni
Nani atakwenda duniani amwokoe mwanadamu
Malaika wote walinyamaza kimya
Wazee ishirini na wanne walinyamaza kimya
Yesu mwana wa Mungu akasema nitakwenda
Kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi
Hata kwa kifo cha aibu kwa ajili yangu na wewe
Alipigwa akadhulumiwa kwa ajili yangu na wewe
Mungu alipotazama hilo akasema amejitoa kwa ajili ya wanadamu
Nimempatia heshima na jina la heshima
Unapotaja jina la Yesu unafunguliwa
Unapotaja jina la Yesu unawekwa huru
Jina la Yesu dawa, jina la Yesu ni dawa
Yabadilisha wenye dhambi, jina la Yesu ni dawa
Yabadilisha makahaba, jina la Yesu ni dawa
Yabadilisha walevi, jina la Yesu ni dawa
Jina la Yesu dawa, jina la Yesu ni dawa
Eh ni dawa, Jina la Yesu dawa
Naona watu wanatembea kwenye giza
Wana macho lakini hawaoni
Wana masikio lakini hawasikii
Wanahangaika wanahangaika
Wanatafuta msaada wa karmazira
vijana wadogo wanatafuta masponsor
Hello hello munisikie
Yesu leo ameinuliwa kama nyoka wa shaba
Nami leo naliinua jina la Yesu
Kwa jina hili viwete wanatembea yoyoo
Kwa jina hili vipofu wapata kuona
kwa jina la Yesu leo tumemuona Bwana
Kwa jina la Yesu leo tumesamehewa dhambi
Kwa jina la Yesu leo tunaitwa wana wa Mungu
Kwa jina la Yesu leo twamutumikia Bwana
Kwa jina la Yesu jina lenye nguvu
Jina hili ni power, jina hili ni moto
Dawa inayosamehe dhambi, jina la Yesu ni dawa
...
Eeh ni dawa yoh yoh, jina la Yesu ni dawa
Ni jawabu la maisha, jina la Yesu ni dawa
Natangazia ulimwengu wote jina la Yesu ni dawa