Chorus / Description :
anajibu maombi
Anajibu maombi yeye ni Mungu wa Miungu
Kama Paulo na Sila walivyofungwa gerezani
Waliomba na kusifu na akajibu maombi yao
Anajibu Maombi , anajibu maombi
Anajibu maombi yeye ni Mungu wa Miungu
Kama Paulo na Sila walivyofungwa gerezani
Waliomba na kusifu na akajibu maombi yao
Na yule lazaro alipokufa walikimbia kumwita Yesu
Yesu akawaambia amelala akamfufua lazaro
Anajibu Maombi, anajibu maombi
Anajibu maombi yeye ni Mungu wa miungu
Anajibu Maombi, anajibu maombi
Anajibu maombi yeye ni Mungu wa miungu
Kumbuka vile Sarah alivyoomba kwa miaka nyingi
Mungu akajibu hilo ombi lake, akambariki na Isaka
Na ile safari ya waisraeli, ilipotatizwa na wamisri
Mungu aliwapasulia bahari na akajibu maombi yao
Anajibu Maombi, anajibu maombi
Anajibu maombi yeye ni Mungu wa miungu
Anajibu Maombi, anajibu maombi
Anajibu maombi yeye ni Mungu wa miungu
Walipomletea Yule kipofu, Yesu alimuekelea mkono
Hapo upofu wake ukaisha, akamshukuru Mungu
Je wamkumbuka yule mwanamke alivyomwaga damu kwa miaka nyingi
Aligusa vazi la Yesu na akajibu ombi lake
Anajibu Maombi, anajibu maombi
Anajibu maombi yeye ni Mungu wa miungu
Anajibu Maombi, anajibu maombi
Anajibu maombi yeye ni Mungu wa miungu