Carole Kirima - Hakuna Kabisa Dawa ya Makosa

Chorus / Description : Sioshwi dhambi zangu, Bila damu yake Yesu.
Hapendezewi Mungu, Bila damu yake Yesu.
Hakuna kabisa Dawa ya makosa
Ya kututakasa, Ila damu yake Yesu.

Hakuna Kabisa Dawa ya Makosa Lyrics

Sioshwi dhambi zangu, Bila damu yake Yesu.
Hapendezewi Mungu, Bila damu yake Yesu.

Hakuna kabisa Dawa ya makosa
Ya kututakasa,Ila damu yake Yesu.

La kunisafi sina Ila damu yake Yesu.
Wala udhuru tena, Ila damu yake Yesu.

Hakuna kabisa Dawa ya makosa
Ya kututakasa,Ila damu yake Yesu.

Sipati pataniswa, Bila damu yake Yesu.
Hukumu yanitisha, Bila damu yake Yesu.

Hakuna kabisa Dawa ya makosa
Ya kututakasa,Ila damu yake Yesu.

Sipati tumaini, Bila damu yake Yesu.
Wema wala amani, Bila damu yake Yesu.

Hakuna kabisa Dawa ya makosa
Ya kututakasa,Ila damu yake Yesu.

Yashinda ulimwengu, Hiyo damu yake Yesu.
Na kutufikisha juu, Hiyo damu yake Yesu.

Hakuna kabisa Dawa ya makosa
Ya kututakasa,Ila damu yake Yesu.

Hakuna Kabisa Dawa ya Makosa Video

  • Song: Hakuna Kabisa Dawa ya Makosa
  • Artist(s): Carole Kirima


Share: