Chorus / Description :
Nitoke nawe, nitoke nawe
Minawe, mina wewe tu
(To Go with You)
Minashindwa nitoke kwenye sanaa nisikike
Nataka unieleze nielewe aah
Ona hata juhudi zangu kagonga mwamba nikafifia
Kimziki sisikii tena,
Ona wananiona sifai kimiziki sina nafasi
Nieleze nifanye nini,
sijui nifanye scandal au wimbo wenye utata nisikike
Au nifanye jingo wanitambue,
No no ila huu mwaka nataka ...
Nitoke nawe, Nitoke nawe
Nitoke nawe, nitoke nawe
Nishike mkono uniongoze aah
Wengi walinidanganya eti niwe kama * wamwonekana
Ndo wenye kiki na umaarufu sana
Wako wapi leo kisichoidhinishwa na Mungu
Hakiwezi kudumu, Yeye ndo mwanzo tena mwisho
Ndio yake ni ndio na amina
Yeye ndiye mwenye kuinua tena kubariki
si lazima nifanye scandal au wimbo wenye utata nisikike
Au nifanye jingo wanitambue ila mwika mi nataka
Nitoke nawe, Nitoke nawe
Nitoke nawe, nitoke nawe
Minawe, mina wewe tu
Minawe, nimechoka na ya wanadamu
Minawe, hata waseme sana
Nitoke Nawe( To Go With You) by Danny Gift