Geraldine Oduor - Msaada Wangu - Zaburi

Chorus / Description : Nitayainua macho yangu milimani
Msaada wangu watoka wapi ?
Msaada wangu kwako Bwana

Msaada Wangu - Zaburi Lyrics

Nitayainua macho yangu milimani
Msaada wangu watoka wapi
Msaada wangu kwako Bwana

Nakuinulia macho yangu
Wewe uketiye juu sana
Kama macho ya watumishi
Wa mkono wa Bwana zao
Nilitewe nuru yako
Kweli azidi kuniongoza
Zinifikishe kwenye mlima
Maskani yako takatifu

Bwana ndiye mlinzi wangu
Uvuli wa mkono wake
Jua halinipigi mchana
Wala mwezi usiku
Anilinda na mabaya
Atalinda nafsi yangu
Nitokapo na niingiapo
Tangu sasa na milele

Nitayainua macho yangu milimani
Msaada wangu watoka wapi?
Msaada wangu kwako Bwana

Sheria yako ni kamilifu
Huiburudisha nafsi yangu
Ushuhuda wako ni amini, hunitia hekima
Maagizo yako ni adili, hufurahisha nafsi yangu
Amri yako ni safi sana, huyatia macho huru

Kilicho chako ni kitakatifu, Kinadumu milele
Hukumu zako ni za kweli, zina haki kabisa
Kuliko wengi wa dhahabu, hukumu zako zatamanika
Kuliko sega za asali, hukumu zako tamu kweli

Nitayainua macho yangu milimani
Msaada wangu watoka wapi?
Msaada wangu kwako Bwana

Bass
Nitayainua macho yangu milimani
Wewe u msaada, wangu wa karibu

Msaada Wangu - Zaburi Video

  • Song: Msaada Wangu - Zaburi
  • Artist(s): Geraldine Oduor


Share: