Chorus / Description :
Mungu ibariki Kenya
takasa iponye irehemu nchi Kenya,
Kama vile milima izungukavyo Yerusalemu
Izunguke izingire Kenya ikumbatie
Mungu bariki Kenya, takasa iponye irehemu nchi Kenya
Kama vile milima izungukavyo yerusalemu
Izunguke izingire Kenya ikumbatie
Mungu twaomba, Mungu ibariki Kenya
takasa iponye irehemu nchi Kenya,
Kama vile milima izungukavyo yerusalemu
Izunguke izingire Kenya ikumbatie
Ulisema iwapo watu wangu walioitwa kwa Jina langu.
Watanyenyekea na kuomba, watafute uso wangu
Waachane na njia zao mbovu nitawasikiaa
Tawasamehe dhambi nchi yao ntaiponya
Mungu twaomba, Mungu ibariki Kenya
takasa iponye irehemu nchi Kenya,
Kama vile milima izungukavyo Yerusalemu
Izunguke izingire Kenya ikumbatie
Sikia vilio vya wajane, futa machozi, futa machozi ya yatima
Maskini na wasiojiweza, ondoa baa la njaa, jangwa tuepushe
Bwana tutee ee.
Boresha uchumi wa nchi, Baba tuinue
Mungu ibariki Kenya
takasa iponye irehemu nchi Kenya,
Kama vile milima izungukavyo Yerusalemu
Izunguke izingire Kenya ikumbatie
Kenya ni yako Baba hatuwezi Bila wewe Mungu wetu, wewe ni tumaini letu
KENYA IMEBARIKIWA
Limebarikiwa taifa Mungu wao ni Mungu,
Halitatikiswa kamwe wima litasimama
Limebarikiwa taifa Mungu wao ni Mungu, Halitatikiswa kamwe
Limebarikiwa taifa Mungu wao ni Mungu, Halitatikiswa kamwe