Chorus / Description :
Wastahili milele na milele
Mungu wetu twakusifu, pokea sifa
Wewe Mungu hulinganishwi, hufananishwi
Na yeyote, uliumba hukuumbwa pokea sifa
"Come on everybody lets give Jesus praise
He is worthy to be praised"
Kwa matendo yako viumbe vyote twakutukuza
Umejawa rehema na neema, muweza yote
Kwa matendo yako viumbe vyote twakutukuza
Umejawa rehema na neema, muweza wa yote
Wastahili milele na milele
Mungu wetu twakusifu, pokea sifa
Mungu wetu twakusifu, mtawala mwaminifu
Mwenye enzi twakuinua, pokea sifa
Wewe Mungu unaponya, wabariki wainua
Wewe pekee twakusifu, pokea sifa
Wastahili wastahili, milele na milele
Mungu wetu twakusifu, pokea sifa
Wewe Mungu hulinganishwi, hufananishwi
Na yeyote, uliumba hukuumbwa pokea sifa
Uweza wako ni wa milele, ufalme wako ni wa milele
Wewe pekee twakusifu, pokea sifa
Wastahili wastahili, milele na milele
Mungu wetu twakusifu, pokea sifa
Kwa matendo yako, viumbe vyote twakutukuza
Umejawa na rehema, neema muweza yote
Kwa matendo yako, viumbe vyote twakutukuza
Umejawa na rehema, neema muweza yote
Wastahili wastahili, milele na milele
Mungu wetu twakusifu, pokea sifa