Chorus / Description :
Mwenyezi mimi nasubiri bado (mwenyezi)
Nasubiri bado (mwenyezi)
Nasubiri bado nangoja kwako (mwenyezi)
Nasubiri bado (mwenyezi)
Kutwa nzima imepita nikiwa ata sina cha mfukoni
Naumia hakika kwani ata marafiki nao siwaoni
Kwenye wingu la giza sijapata ata faraja tumboni
Koroboi ndo stima namweleza yule unayetoka moyoni
Maisha haya kizunguzungu ni wapi tena sina pakutorokea
Kwenye giza sioni nuru ni nini chanzo nabaki nikijiongelea
Kama namwona mamangu uchochole ndio wimbo na ndo kikwazo
Pekee yangu kwa hakika naangaziwa sana
Machozi ndo yangu hata kunivika cha chini ndio langu pato
Eeeh mola wangu eeeh eeh
Mwenyezi mimi nasubiri bado (mwenyezi)
Nasubiri bado (mwenyezi)
Nasubiri bado nangoja kwako (mwenyezi)
Nasubiri bado (mwenyezi)
Nasubiri bado (mwenyezi)
Nasubiri bado nangoja kwako (mwenyezi)
Mbona mawazo yangu ndo hivo katu sichoki kufikiria
Masikini moyo wangu
Mzigo wangu ndo mzito sina ata wa kunisaidia
Naja kwako mola wangu maumivu yangu yaokolee
Toka zama sichoki kusota dili zangu zakutege
Mara napata saa zingine nakosa nyumbani nategemewa
Wamechoka wa kunikopesha wazidi niombea wasikate tamaa
oooh ooh oooh
Kama kufunga sio mwanzo ni mtindo mpaka nashindwa nini ndo chanzo
Ndio maana nimeandika wimbo
Matatizo yasiyokosa likizo kilio ndio yangu mtindo
Ni maji yamefika kwa shingo aaih
Kama namwona mamangu uchochole ndio wimbo na ndo kikwazo
Pekee yangu kwa hakika naangaziwa sana
Machozi ndo yangu hata kunivika cha chini ndio langu pato
Eeeh mola wangu eeeh eeh
Mwenyezi mimi nasubiri bado (mwenyezi)
Nasubiri bado (mwenyezi)
Nasubiri bado nangoja kwako (mwenyezi)
Nasubiri bado (mwenyezi)
Nasubiri bado (mwenyezi)
Nasubiri bado nangoja kwako (mwenyezi)
Kupambana kidume sichoki
Sala zangu nitume sichoki
Siwasikizi wengine sichoki
Ipo siku ntapata