Chorus / Description :
Achana nao ah, Achana nao eeh
Wapakwa mafuta ni wateule achana nao
Achana nao ah, Achana nao eeh eh
Walioitanishwa kwa jina la Baba achana nao
Kazi ya kupigana na watu wa Mungu achana nayo
Wapakwa mafuta ni wateule achana nao
Vita vyao ni Mungu mwenyewe anawapigania eeh
Wamezingirwa na moto cheza mbali nao
Achana nao ah, Achana nao eeh
Wapakwa mafuta ni wateule achana nao
Achana nao ah, Achana nao eeh eh
Walioitanishwa kwa jina la Baba achana nao
Sauli kwa unafiki aliokuwa nayo
Alipanga vita kinyume na mtu wa Mungu Daudi
Hakujua vita vya Daudi ni vyake Mungu eeh
Mungu alimleta Sauli hadi mikononi mwa Daudi
Daudi alikata vazi la Sauli kisha akamuonyesha
Akamwambia tazama ningetaka ningekuangamiza ah
Sauli kutazama akapiga magoti akatoa machozi
Hapo akatambua wapakwa mafuta achana nao
Vita vyao ni Mungu mwenyewe anawapigania ah eh
Achana nao ah, Achana nao eeh
Wapakwa mafuta ni wateule achana nao
Achana nao ah, Achana nao eeh eh
Walioitanishwa kwa jina la Baba achana nao
Kuna watu wameitwa wamepakwa mafuta
Kwa kazi ya Bwana wamejitoa kwa hali na mali
Lakini bado kukataliwa kushushwa moyo
kuonewa bure, kushushwa chini, kudharauliwa
Ewe usife moyo, kwani tunaye Mungu
Ewe usife moyo, kwani tunaye Mungu
Vita vyetu ni Mungu mwenyewe atupigania
Achana nao ah, Achana nao eeh
Wapakwa mafuta ni wateule achana nao
Achana nao ah, Achana nao eeh eh
Walioitanishwa kwa jina la Baba achana nao
Ninamwita Mungu wa akina Shadrack akupiganie
Kwenye moto ya majaribu usichomeke
Ninamwita Mungu wa Danieli akupiganie wewe
Afunge midomo ya adui zako uishi salama
Ninamwita Mungu wa Israeli akupiganie eeh
Afanye njia mahali ambapo hapana njia
Wapendwa msife moyo kwani tunaye Mungu
Achana nao ah, Achana nao eeh
Wapakwa mafuta ni wateule achana nao
Achana nao ah, Achana nao eeh eh
Walioitanishwa kwa jina la Baba achana nao
Achana nao ah, Achana nao eeh
Wapakwa mafuta ni wateule achana nao
Achana nao ah, Achana nao eeh eh
Walioitanishwa kwa jina la Baba achana nao