Solomon Mukubwa - Mungu wetu Mwenye Nguvu Baba wa milele

Chorus / Description : Mungu wetu mwenye nguvu Baba wa milele
eeh ni MWenye Nguvu, Ebenzer Baba wa milele
Maneno yako yana nguvu sana, yana nguvu sana
Baba utukuzwe Baba uinuliwe

Mungu wetu Mwenye Nguvu Baba wa milele Lyrics

Biblia yasema waabudio Bwana wataabudu katika roho na Kweli, na ni wakati huu ukiwa ndani ya gari lako ukiwa ndani ya Basi unasafiri, ukiwa unafanya kazi ndani ya ofisi yako, jiunge pamoja nami tumwinue tumwambie wastahili uko mwenye nguvu. Ikiwa uliamka asubuhi na hukumwambia kitu Mungu ni wakati wa kumwambia utukuzwe, uinuliwe, jiunge pamoja tumwambie wastahili. Ikiwa unakuwa kwenye maombi ya kufunga na kuomba hebu jiunge pamoja nasi, twende...

Mungu wetu mwenye nguvu Baba wa milele
Mungu wetu mwenye nguvu Baba wa milele
eeh ni MWenye Nguvu, Ebenzer Baba wa milele
Mungu wetu mwenye nguvu Baba wa milele
Ehe wanipa mema, Baba wa milele yote
Mungu wetu mwenye nguvu Baba wa milele
Nguvu zako zashangaza dunia
uliumba mbingu pasipo nguzo hewani Baba
Mungu wetu mwenye nguvu Baba wa milele

Uko mwema Bwana matendo yako ni ya ajabu sana
Neema yako fadhili zako kila asubuhi
Ni mpya tena zanifajiri Mungu niamu kapo
Nikosewa na maisha wanipa tumaini la kupata maisha
Wajapo nicheka majirani wangu wewe ni kwa upande wangu
Ooh Baba, Neema yako fadhili zako kila asubuhi
Ni mpya tena zanifajiri Mungu niamukapo
Wanipa tumaini la Maisha Baba yangu duniani
Natembea nawe Baba yangu hujaniacha mimi
Neema yako fadhili zako kila asubuhi
Ni mpya tena zanifajiri Mungu niamukapo
Kulala kuamuka ni kwa neema yake Mungu ndugu yangu
Ulimupa Mungu nini wewe, usione jinsi ulivyo,
usijivune vune ni neema yake Mungu
Neema yako fadhili zako kila asubuhi
Ni mpya tena zanifajiri Mungu niamukapo

Nani kama wewe Mungu, sina mwingine kama wewe
Mfalme wa dunia ni wewe, mwanzo na mwisho ni wewe
Baba utukuzwe Baba uinuliwe
Daddy Daddy, Baba utukuzwe Baba uinuliwe
Rafiki yangu I love you, I love you, I love you Baba yoo
Baba utukuzwe Baba uinuliwe
Maneno yako yafungua watu, yafungua waatu
Baba utukuzwe Baba uinuliwe
Sitasahau ulikonitoa umenitoa mbali, umenitoa mbali
Baba utukuzwe Baba uinuliwe
Rafiki yangu nakupenda sana, nakupenda sana
Baba utukuzwe Baba uinuliwe
Maneno yako yana nguvu sana, yana nguvu sana
Baba utukuzwe Baba uinuliwe
Kwa neno lako lazaro kafufuka, kafufuka
Baba utukuzwe Baba uinuliwe
Oh Baba, Oh Baba, Oh baba

Mungu wetu Mwenye Nguvu Baba wa milele Video

  • Song: Mungu wetu Mwenye Nguvu Baba wa milele
  • Artist(s): Solomon Mukubwa


Share: