Msalabani pa Mwokozi (Tenzi 77) Lyrics

Msalabani pa mwokozi, hapo niliomba upozi,
akaniokoa mpenzi, mwana wa Mungu.

Mwana wa Mungu, mwokozi wangu,
akaniokoa mpenzi, mwana wa Mungu

Chini ya mti msumbufu, niliomba utakatifu,
alinikomboa kwa damu, mwana wa Mungu.

Aliniokoa dhambini, ikawa kunikaa ndani,
aliponifia mtini, mwana wa Mungu.

Damu ya Yesu ya thamani, huniokoa makosani,
huniendesha wokovuni, mwana wa Mungu.

Hicho kijito cha gharama, leo jivike kwa kuzama,
kwake uuone uzima, mwana wa Mungu.

Msalabani pa Mwokozi (Tenzi 77) Video


MSALABANI PA MWOKOZI. TENZI NAMBA 77. Video.Share:

Write a review/comment/correct the lyrics of Msalabani Pa Mwokozi (tenzi 77):

0 Comments/Reviews