23 Ni Salama Rohoni Mwangu Lyrics

By Sheddy

Lyrics

Nionapo amani kama shwari, ama nionapo shida;
Kwa mambo yote umenijulisha, ni salama rohoni mwangu.

Salama, rohoni, ni salama rohoni mwangu!

Ingawa shetani atanitesa, nitajipa moyo
kwani Kristo ameona unyonge wangu, amekufa kwa roho yangu. .

Salama, rohoni, ni salama rohoni mwangu!

Dhambi zangu zote, wala si nusu, zimewekwa msalabani;
Wala sichukui laana yake, ni salama rohoni mwangu

Salama, rohoni, ni salama rohoni mwangu!

Ee Bwana himiza siku ya kuja, panda itakapolia;
utakaposhuka sitaogopa, ni salama rohoni mwangu.

Salama, rohoni, ni salama rohoni mwangu!
Hymn
It is well with my soul

Sheddy - Salama Rohoni (Tenzi za rohoni)

Now Playing...