Nyimbo Za Kristo - Twendeni Askari

Chorus / Description : Twende askari watu wa Mungu;
Yesu yuko Mbele, tumwandame juu.
Onward Christian Soldiers in kiSwahili hymn

Twendeni Askari Lyrics

Twendeni askari, watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele, tumwandame juu.
Ametangulia Bwana vitani, twende mbele kwani ndiye amini.

Twende askari watu wa Mungu;
Yesu yuko Mbele, tumwandame juu.

Jeshi la Shetani, likisikia jina la Mwokozi,
litakimbia, kelele za shangwe zivume nchi; n
dugu inueni zenu sauti.

Twende askari watu wa Mungu;
Yesu yuko Mbele, tumwandame juu.

Kweli kundi dogo, watu wa Mungu sisi na mababa tu moja fungu.
Hatutengwi nao, moja imani, Tumaini moja, na moja dini.

Twende askari watu wa Mungu;
Yesu yuko Mbele, tumwandame juu.

Haya mbele watu nasi njiani, inueni myoyo, nanyi sifuni;
heshima na sifa ni ya Mfalme, juu hata chini, sana zivume. .
 Onward Christian Soldiers Swahili Version

Twendeni Askari Video

  • Song: Twendeni Askari
  • Artist(s): Nyimbo Za Kristo


Share: