Chorus / Description :
Kumbe Mungu aniona, macho yako yanitazama
Sikio lako lanisikia, siwezi jificha aah
Mbele ya macho ya wanadamu
Nilikuwa nikijificha
Kumbe wewe waniona
Kwa Kujifanya (mtakatifu) tena (mkarimu)
Nilikuwa (mnyenyekevu tena mpole sana)

Kwenye ibada (mnyenyekevu tena mpole sana)
Kama Mungu angechagua watu wake
Mimi singekuwepo duniani
Kama Mungu angechagua watakatifu
Mimi singekuwepo duniani
Mimi binadamu wala si malaika
Mengi ninakosea na kukuchukiza
Ninafanya mambo yasiyostahili
Nimevuruga-vuruga mipango yako
Wanihurumia,
Mbele ya macho ya wanadamu
Nilikuwa nikijificha
Kumbe wewe waniona
Kwa Kujifanya (mtakatifu) tena (mkarimu)
Nilikuwa (mnyenyekevu tena mpole sana)
Kwa Kujifanya (mtakatifu) tena (mkarimu)
Kwenye ibada (mnyenyekevu tena mpole sana)
Kumbe Mungu aniona, macho yako yanitazama
Sikio lako lanisikia, siwezi jificha aah
Kumbe Mungu aniona, macho yako yanitazama
Sikio lako lanisikia, siwezi jificha aah
Sasa nimetambua mbivu na mbichi ni zipi
Sasa ninaelewa njia salama ni wapi
Na nimejua bila ya wewe sifiki
Hata nikila pasipo neno lako sishibi
Neema yako (ila kwa neema yako)
Upendo wako (ila kwa upendo wako)
Na rehema zako zimenihimarisha tena