Zabron Singers - Imenigharimu

Chorus / Description : Imenigharimu sana mimi kuwa hapa
Wacha Mungu awe Mungu
Tangu kuzaliwa kwangu, ujana, uzee
Hajawai mi niacha

Imenigharimu Lyrics

Imenigharimu sana mimi kuwa hapa 
Wacha Mungu awe Mungu 
Tangu kuzaliwa kwangu ujana uzee 
Hajawai mi niacha 

Kwenye giza kaniwekea nuru nisihangaike 
Kwenye shida hutengeneza njia watu wake tunapita
Nimekuja kugundua umbali umenileta 
Acha Mungu nikusifu 

Mimi sina Mungu mwingine wa kunitendea haya 
Hakika wanikumbuka 
Hivi nilivyo Mungu ni yeye kaniwezesha 
Ni muweza Baba heehee
Ntaendela kuvuka popote niko na Mungu 
Ni Mungu yuko na mimi 

Ni mengi nimepitia na leo kufika hapa 
Kama si Mungu ni nani? Wadhani nani tena 
Mengi akanivusha na baraka zikapanda 
Wadhani Mungu ni nani, ni nani

Yeye ni nani, wadhani ni nani 
Mungu ni nani eeh eeh

Kuzihesabu tu siku ni nguvu za Mungu 
Ndio maana niko hai 
Sikumlipa chochote, 
wakati wa Mungu unapofika umefika 

Nilipokuita hukusita, ulisema nami 
Ninakushukuru umenipa maisha mazuri  

Nimekuja kugundua wewe ni Mungu mwenye nguvu 
Mwenye mamlaka yote 
Sababu niko na wewe sina hofu na mashaka 
Vita si yangu ni yako 

Hivi nilivyo Mungu ni yeye kaniwezesha 
Ni muweza Baba heehee
Ntaendela kuvuka popote niko na Mungu 
Ni Mungu yuko na mimi 

Ni mengi nimepitia na leo kufika hapa 
Kama si Mungu ni nani? Wadhani nani tena 
Mengi akanivusha na baraka zikapanda 
Wadhani Mungu ni nani, ni nani

Utabaki kuwa Mungu uu

Imenigharimu Video

  • Song: Imenigharimu
  • Artist(s): Zabron Singers


Share: