Solomon Mukubwa - Habari Njema Raha Yangu - Ndiyo Dhamana

Chorus / Description : Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu.

Habari Njema Raha Yangu - Ndiyo Dhamana Lyrics

Ndiyo dhamana, Yesu wangu,
Hunipa furaha za mbingu,
Mrithi wa wokovu wake,
Nimezawa kwa roho wake.

Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu.

Kumsalimu moyo wangu,
Mara namwona raha yangu,
Aniletea malaika,
Wanilinda, taokoka.

Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu.

Sina kinyume; nashukuru,
Mchana kutwa huja kwangu,
Usiku kucha kuna nuru,
Mwokozi wangu; ndimi nuru.

Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu.

Hali na mali, anitwaa!
Mara namwona anifaa,
Nami nangonja kwa subira,
Akiniita nije mara.

Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu.

Habari Njema Raha Yangu - Ndiyo Dhamana Video

  • Song: Habari Njema Raha Yangu - Ndiyo Dhamana
  • Artist(s): Solomon Mukubwa


Share: