1 Samweli Mlango 29 1st Samuel

1 Samweli 29:1 1stSamuel 29:1

Basi hao Wafilisti wakakusanya majeshi yao yote huko Afeki; nao Waisraeli wakafanya kambi karibu na chemchemi iliyoko Yezreeli.

1 Samweli 29:2 1stSamuel 29:2

Nao mashehe wa Wafilisti wakapita mbele, mia kwa mia, na elfu kwa elfu; naye Daudi na watu wake wakapita wa mwisho pamoja na Akishi.

1 Samweli 29:3 1stSamuel 29:3

Ndipo wakuu wa Wafilisti wakasema, Waebrania hawa wafanyani hapa? Naye Akishi akawaambia wakuu wa Wafilisti, Je! Siye huyu Daudi, yule mtumishi wa Sauli, mfalme wa Israeli, ambaye amefuatana na mimi siku hizi, naam, miaka hii, wala mimi nisione hatia kwake, tangu hapo aliponiangukia mimi hata leo?

1 Samweli 29:4 1stSamuel 29:4

Lakini wakuu wa Wafilisti wakamkasirikia; nao wakuu wa Wafilisti wakamwambia, Mrudishe huyu, apate kurejea mahali pake ulipomwagiza, wala asiende pamoja nasi vitani, asije akawa adui wetu vitani; kwani mtu huyu angejipatanisha na bwana wake kwa njia gani? Je! Si kwa vichwa vya watu hawa?

1 Samweli 29:5 1stSamuel 29:5

Je! Siye huyo Daudi, ambaye waliimbiana habari zake katika michezo, wakisema,Sauli amewaua elfu zake,Na Daudi makumi elfu yake?

1 Samweli 29:6 1stSamuel 29:6

Ndipo Akishi akamwita Daudi, akamwambia, Aishivyo Bwana, wewe umekuwa mwenye adili, tena kutoka kwako na kuingia kwako pamoja nami katika jeshi ni kwema machoni pangu; kwa sababu mimi sikuona uovu ndani yako tangu siku ile uliponijia hata leo; walakini hao wakuu hawakuridhii.

1 Samweli 29:7 1stSamuel 29:7

Basi sasa urudi, uende zako kwa amani, ili usiwachukize hao mashehe wa Wafilisti.

1 Samweli 29:8 1stSamuel 29:8

Naye Daudi akamwambia Akishi, Lakini mimi nimefanyaje? Nawe umeona nini kwangu mimi mtumwa wako, muda wote niliokaa mbele yako hata leo, nisipate ruhusa niende na kupigana na adui za bwana wangu mfalme?

1 Samweli 29:9 1stSamuel 29:9

Akishi akajibu, akamwambia Daudi, Mimi najua ya kuwa u mwema machoni pangu, kama malaika wa Mungu; ila hao wakuu wa Wafilisti wamesema, Huyu hatakwea pamoja nasi kwenda vitani.

1 Samweli 29:10 1stSamuel 29:10

Kwa hiyo sasa amka asubuhi na mapema, wewe na watumwa wa bwana wako waliokuja pamoja nawe; nanyi mtakapoamka asubuhi na mapema, na kupata mwanga, nendeni zenu.

1 Samweli 29:11 1stSamuel 29:11

Basi Daudi akaamka asubuhi na mapema, yeye na watu wake, kwenda zao asubuhi, kuirudia nchi ya Wafilisti. Nao Wafilisti wakakwea kwenda Yezreeli.