2 Yohana Mlango 1 2nd John

2 Yohana 1:1 2ndJohn 1:1

Mzee, kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuao ile kweli;

2 Yohana 1:2 2ndJohn 1:2

kwa ajili ya hiyo kweli ikaayo ndani yetu, nayo itakuwa pamoja nasi hata milele.

2 Yohana 1:3 2ndJohn 1:3

Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo Mwana wa Baba, zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.

2 Yohana 1:4 2ndJohn 1:4

Nalifurahi mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba.

2 Yohana 1:5 2ndJohn 1:5

Na sasa mama, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.

2 Yohana 1:6 2ndJohn 1:6

Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo.

2 Yohana 1:7 2ndJohn 1:7

Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo.

2 Yohana 1:8 2ndJohn 1:8

Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu.

2 Yohana 1:9 2ndJohn 1:9

Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia.

2 Yohana 1:10 2ndJohn 1:10

Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.

2 Yohana 1:11 2ndJohn 1:11

Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu.

2 Yohana 1:12 2ndJohn 1:12

Kwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini nataraji kuja kwenu, na kusema nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu iwe imetimizwa.

2 Yohana 1:13 2ndJohn 1:13

Watoto wa ndugu yako aliye mteule, wakusalimu.