Habakuki Mlango 3 Habakkuk

Habakuki 3:1 Habakkuk 3:1

Sala ya nabii Habakuki.

Habakuki 3:2 Habakkuk 3:2

Ee Bwana, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee Bwana, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema.

Habakuki 3:3 Habakkuk 3:3

Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.

Habakuki 3:4 Habakkuk 3:4

Mwangaza wake ulikuwa kama nuru; Alikuwa na mishale ya nuru ubavuni pake; Ndipo ulipofichwa uweza wake.

Habakuki 3:5 Habakkuk 3:5

Mbele zake ilikwenda tauni, Na makaa ya moto yakatoka miguuni pake.

Habakuki 3:6 Habakkuk 3:6

Akasimama, akaitetemesha dunia; Akatazama, akawasitusha mataifa; Na milima ya zamani ikatawanyika; Vilima vya kale vikainama; Miendo yake ilikuwa kama siku za kale.

Habakuki 3:7 Habakkuk 3:7

Naliziona hema za Kushani katika taabu; Mapazia ya nchi ya Midiani yakatetemeka.

Habakuki 3:8 Habakkuk 3:8

Je! Bwana aliikasirikia mito? Je! Hasira yako ilikuwa juu ya mito, Au ghadhabu yako juu ya bahari, Hata ukapanda farasi zako, Katika magari yako ya wokovu?

Habakuki 3:9 Habakkuk 3:9

Uta wako ukafanywa wazi kabisa; Viapo walivyopewa kabila vilikuwa neno thabiti; Ukaipasua nchi kwa mito.

Habakuki 3:10 Habakkuk 3:10

Milima ilikuona, ikaogopa; Gharika ya maji ikapita; Vilindi vikatoa sauti yake, Vikainua juu mikono yake.

Habakuki 3:11 Habakkuk 3:11

Jua na mwezi vikasimama makaoni mwao; Mbele ya nuru ya mishale yako ilipotapakaa, Mbele ya mwangaza wa mkuki wako umeremetao.

Habakuki 3:12 Habakkuk 3:12

Ulikwenda katikati ya nchi kwa ghadhabu; Ukawapura mataifa kwa hasira.

Habakuki 3:13 Habakkuk 3:13

Ukatokea kwa ajili ya wokovu wa watu wako, Kwa ajili ya wokovu wa masihi wako; Ukakiponda kichwa cha nyumba ya waovu, Ukiuweka wazi msingi hata mwambani.

Habakuki 3:14 Habakkuk 3:14

Ukakichoma kichwa cha mashujaa wake kwa fimbo zao wenyewe; Wakaja kama kisulisuli ili kunitawanya; Kama wakifurahi kuwameza maskini kwa siri.

Habakuki 3:15 Habakkuk 3:15

Ukaikanyaga bahari kwa farasi zako, Chungu ya maji yenye nguvu.

Habakuki 3:16 Habakkuk 3:16

Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka, Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile; Ubovu ukaingia mifupani mwangu, Nikatetemeka katika mahali pangu; Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki, Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu.

Habakuki 3:17 Habakkuk 3:17

Maana mtini hautachanua maua, Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng'ombe;

Habakuki 3:18 Habakkuk 3:18

Walakini nitamfurahia Bwana Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.

Habakuki 3:19 Habakkuk 3:19

YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.