Waebrania Mlango 5 Hebrews

Waebrania 5:1 Hebrews 5:1

Maana kila kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya wanadamu katika mambo yamhusuyo Mungu, ili atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi;

Waebrania 5:2 Hebrews 5:2

awezaye kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe yu katika hali ya udhaifu;

Waebrania 5:3 Hebrews 5:3

na kwa sababu hiyo imempasa, kama kwa ajili ya watu, vivyo hivyo kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi.

Waebrania 5:4 Hebrews 5:4

Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni.

Waebrania 5:5 Hebrews 5:5

Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.

Waebrania 5:6 Hebrews 5:6

kama asemavyo mahali pengine, Ndiwe kuhani wa milele Kwa mfano wa Melkizedeki.

Waebrania 5:7 Hebrews 5:7

Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;

Waebrania 5:8 Hebrews 5:8

na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata;

Waebrania 5:9 Hebrews 5:9

naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;

Waebrania 5:10 Hebrews 5:10

kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.

Waebrania 5:11 Hebrews 5:11

Ambaye tuna maneno mengi ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia.

Waebrania 5:12 Hebrews 5:12

Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu.

Waebrania 5:13 Hebrews 5:13

Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga.

Waebrania 5:14 Hebrews 5:14

Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.