Msalaba ndio asili ya mema Lyrics

By Angela Chibalonza

Lyrics

Sioni haya kwa Bwana,
Kwake nitang’ara!
Mti wake sitakana,
Ni neno imara.

(Chorus)
Msalaba ndio asili ya mema,
Nikatua mzigo hapo;
Nina uzima, furaha daima,
Njoni kafurahini papo.

Kama kiti chake vivyo,
Ni yake ahadi;
Alivyowekewa navyo,
Kamwe, havirudi.

Bwana wangu, tena Mungu,
Ndilo lake jina!
Hataacha roho yangu,
Wala kunikana.

Atakiri langu jina,
Mbele za Babaye,
Anipe pahali tena,
Mbinguni nikae

# At the Cross

"Angela chibalonza || sioni haya \/\/ msalaba\/\/ piano tutorial"

Now Playing...