The Saints Ministers - Amini

Chorus / Description : Amini amini,
amini Yesu amini
Amini amini
Maombi yako yako yatajibiwa

Amini Lyrics

Sijui sababu ya neema aah 
Niliyopewa na Mungu wetu uuh 
Sikustahili pendo lake eeh 
Wala wokovu wa Yesu kristo 

Amini amini, 
amini Yesu amini 
Amini amini
Maombi yako yako yatajibiwa 

Sijui jinsi nilivyopewa 
Imani ya kumwamini Yesu kristo 
Neno lake Yesu lilileta amani yake moyoni mwangu 

Amini amini, 
amini Yesu amini 
Amini amini 
Maombi yako yako yatajibiwa 

Sijui jinsi roho wa Mungu 
Awaonyeshavyo watu wake 
Wapate kuzitambua dhambi 
Na kufuata Yesu mkombozi 

Amini amini, 
amini Yesu amini 
Amini amini 
Maombi yako yako yatajibiwa 

Sijui kama mambo yajayo 
Yatakuwa ya salama kwangu 
Lakini ninamwamini Yesu 
Mpaka tutaonana naye 

Amini amini, 
amini Yesu amini 
Amini amini 
Maombi yako yako yatajibiwa 

Sijui siku gani ya Bwana 
Hapa atakaporudi kwetu 
Nitamngojea kwa imani 
Hata kumlaki hewani mwisho 

Amini amini, 
amini Yesu amini 
Amini amini 
Maombi yako yako yatajibiwa 

Amini Video

  • Song: Amini
  • Artist(s): The Saints Ministers


Share: