Chorus / Description :
Mateso yake Yesu ilikuwa ni huzuni
Mwana wa Mungu kafa bila hatia yeyote
Ili mimi na wewe tuhesabiwe haki
Kwa kupigwa kwako tumepona
Msalabani yote yamekwisha
Kwa kupigwa kwako tumepona
Msalabani yote yamekwisha
Nikikumbuka mateso yake Yesu
Alivyoteseka pale msalabani.
Fimbo, misumari, taji ya miba
Mkuki ubavuni na kutemewa mate.
Mateso yake Yesu ilikuwa ni huzuni
Mwana wa Mungu kafa bila hatia yeyote
Ili mimi na wewe tuhesabiwe haki
(rudia)
Wakamkamata Yesu kama mwizi
Na kumdharau Yesu mwana wa Mungu.
Wakamkamata kama mwizi
Wakumdharau Bwana mwana wa Mungu.
Wakadhani kuwa ndio mwisho
Kumbe ndio mwanzo wa wokovu wangu
Kumbe ndio mwanzo wa wokovu wetu.
Mateso yake Yesu ilikuwa ni huzuni
Mwana wa Mungu kafa bila hatia yeyote
Ili mimi na wewe tuhesabiwe haki
(rudia)
Akasulubiwa Yesu Ju ya msalaba
Akasema Baba, Baba oh wasamehe
Kwani hawajui walitendalo oh ooh
Ndipo Bwana wangu akakata roho
Ndipo Bwana wangu akakata roho
Kwa kupigwa kwako tumepona
Msalabani yote yamekwisha
Kwa kupigwa kwako tumepona
Msalabani yote yamekwisha
Mateso yake Yesu ilikuwa ni huzuni
Mwana wa Mungu kafa bila hatia yeyote
Ili mimi na wewe tuhesabiwe haki