Erick Smith - Si ya Kawaida

Chorus / Description :
Kwamba neema si ya kawaida, imenitoa kwa laana
Hakuna chochote ningefanya mimi ili nikubaliwe na Mungu
Damu yako ya dhamana imeniepusha na hukumu.
Rehema upendo zimeniwezesha kuingia kwa Baba

Si ya Kawaida Lyrics

Nilikuwa wa kudharauliwa
ukanipa heshima Bwana, sijui niseme nini,
Hakuna chochote kile ninaweza jivunia, Isipokuwa neema yako.

Usingelikuwepo nisingelikuwepo
Nisingelipata mimi upendo kama wako

Kwamba neema si ya kawaida, imenitoa kwa laana
Hakuna chochote ningefanya mimi ili nikubaliwe na Mungu
Damu yako ya dhamana imeniepusha na hukumu.
Rehema upendo zimeniwezesha kuingia kwa Baba.

Usingelijitoa ningekuwa wapi
Kwa kupigwa kwako tumepona aa.
Ulibeba mateso shida zote msalabani
Ukasema kuwa yote yamekwisha aa aah.

Usingelikuwepo nisingelikuwepo
Nisingelipata upendo kama wako

Kwamba neema si ya kawaida, imenitoa kwa laana
Hakuna chochote ningefanya mimi ili nikubaliwe na Mungu
Damu yako ya dhamana imeniepusha na hukumu.
Rehema upendo zimeniwezesha kuingia kwa Baba.

Kwamba neema si ya kawaida, imenitoa kwa laana
Hakuna chochote ningefanya mimi ili nikubaliwe na Mungu
Damu yako ya dhamana imeniepusha na hukumu.
Rehema upendo zimeniwezesha kuingia kwa Baba.

Si ya Kawaida Video

  • Song: Si ya Kawaida
  • Artist(s): Erick Smith

Share: