Magena Main Youth Choir - Ombi Langu

Chorus / Description : Mtakatifu Mungu mwenyezi,
Alfajiri sifa zako tutaimba.
Malaika wengi wanakuabudu,
Elfu maelfu wanakusujudu.
Ingawa giza linatuficha fahari tusione,
Wewe utatuwezesha mbinguni makao ya raha.

Ombi Langu Lyrics

Ombi langu Bwana nifike kwako,
Ingawa njia zangu ni nyembamba. 
Nitembee nawe mwokozi wangu, 
Dhoruba zijapo nitazishinda. 

Mtakatifu Mungu mwenyezi, 
Alfajiri sifa zako tutaimba. 
Malaika wengi wanakuabudu, 
Elfu maelfu wanakusujudu. 
Ingawa giza linatuficha fahari tusione, 
Wewe utatuwezesha mbinguni makao ya raha. 

Nitembee nawe Mungu, 
Unene nami kwa upole. 
Ingawa njia sioni pana dhoruba baharini, 
Mitego ya miguu elfu ukinishika mkono, 
Anasa kwangu hasara tautika msalaba. 
Hata mji wa Zayuni nitapata pumziko. 
Hata mji wa Zayuni nitapata pumziko.

Kule mji wa zayuni (nitapata pumziko) 
Kwetu mji wa zayuni (nitapata pumziko) 
Kule mji wa zayuni (nitapata pumziko) 
Kwetu mji wa zayuni (nitapata pumziko) 

Mtakatifu Mungu mwenyezi, 
Alfajiri sifa zako tutaimba. 
Malaika wengi wanakuabudu, 
Elfu maelfu wanakusujudu. 
Ingawa giza linatuficha fahari tusione, 
Wewe utatuwezesha mbinguni makao ya raha. 

Ombi Langu Video

  • Song: Ombi Langu
  • Artist(s): Magena Main Youth Choir


Share: