Mariam Martha - Mimi ni Mama

Chorus / Description : Mimi ni mama, mimi ni mama,
Mimi ni mama, nalilia watoto wangu.
Mimi ni mama, mimi ni mama,
Mimi ni mama, najutia kosa langu.

Mimi ni mama kwa wote wenye mwili
Mimi ni mama kwa wakubwa kwa wadogo
Mimi ni eva mimi ni awa
Naomboleza najutia kosa langu

Mimi ni Mama Lyrics

Oiyee oiyee nalia nalia mimi mzazi
Mimi ni mama, mimi ni mama
Mimi ni mama, nalilia watoto wangu
Mimi ni mama, mimi ni mama
Mimi ni mama, najutia kosa langu

Mimi ni mama kwa wote wenye mwili
Mimi ni mama kwa wakubwa kwa wadogo
Mimi ni eva mimi ni awa
Naomboleza najutia kosa langu
Baba yangu Mungu niangalie leo
Nimekuja kwako kwa huzuni nyingi
Ni kweli baba uliniamini mimi
Ukanipa dunia niwe mama wa wote
Nilikosea sana nilipokula tunda
Ulionikataza ninajuta leo
Matokeo ya dhambi niliyoifanya
inatesa watoto wangu niliyowazaa

Mimi ni mama, mimi ni mama
Mimi ni mama, nalilia watoto wangu
Mimi ni mama, mimi ni mama
Mimi ni mama, najutia kosa langu

Waliotoka tumboni mwangu
tazama sasa baba hawaelewani
Caini huyu anamuua Abeli
Watoto wangu wanamalizana
Mbio za shilingi zamaliza watoto wangu
Wengine kwa risasi wengine kwa mabomu
Wengine wako magerezani
Baba Mungu okoa watoto wetu
Wengine wafaa mahosipitalini,
Hawana shilingi ya kununua kidonge.
Tazama wengine wako uchochoroni,
Hawaendi shule wanacheza gemu.

Mimi ni mama, mimi ni mama,
Mimi ni mama, nalilia watoto wangu.
Mimi ni mama, mimi ni mama,
Mimi ni mama, najutia kosa langu.

Uchungu waniuma nikiwaona watoto
Wanavyoteseka katika dunia hii
Nalilia binti zangu waja wazito
Wamejaa makovu katika tumbo yao
Mara pressure mara kifafa
wapoteza maisha katika uzazi
Neno lako lasema tutazaa kwa uchungu
Operesheni hizi zinatoka wapi
Kina mama wote njoni tuomboleze
Tuwalilie watoto wetu wasiangamie
Tuombee ndoa tuombe amani
Ya nchi yetu isije toweka
Neno linasema waiteni wanawake
Waliostadi kwa kuomboleza
Wawefundisha mabinti zao kuomboleza
Machozi yao yabubujike
Kwa maana mauti imepandia dirishani
Ipate kukatilia mbali watoto wetu
Bwana wangu Yesu wewe ulisema
Enye kina mama msinililie mimi
Bali jililieni nafsi zenu na watoto wenyu

Mimi ni mama, mimi ni mama,
Mimi ni mama, nalilia watoto wangu.
Mimi ni mama, mimi ni mama,
Mimi ni mama, najutia kosa langu.

Mimi ni baba, mimi ni baba
Mimi ni baba, najutia watoto wangu.
Mimi ni baba, mimi ni baba
Mimi ni baba, naombea watoto wangu.

Naombea nchi yangu Tanzania
Naombea kizazi chetu ooh Yesu Africa
Ombea Dunia yote

Mimi ni mama, mimi ni mama,
Mimi ni mama, nalilia watoto wangu.
Mimi ni mama, mimi ni mama,
Mimi ni mama, najutia kosa langu.

Mimi ni Mama Video

  • Song: Mimi ni Mama
  • Artist(s): Mariam Martha


Share: