Chorus / Description :
Wewe ni Baba mwema kwangu, wewe ni Baba
Uhimidiwe Mungu wangu, wewe ni Baba ah
Nikitafakari jinsi Mungu Alivyonipenda mimi
Hata kunithamini mimi niliyedharauliwa na watu
Nikitafakari jinsi Mungu Alivyonipenda mimi
Nikitafakari jinsi Mungu Alivyonipenda mimi
Hata kunithamini mimi niliyedharauliwa na watu
Hata kunithamini mimi niliyedharauliwa na watu . .
Kweli nimejua Mungu wangu, Yeye sio mwanadamu (x2)
Kama angekuwa mwanadamu, nisingefika leo (x2)
Maana katika kilio changu wengi walinitenga
Maana katika machozi yangu wengi walinitenga
Sikumwona hata mpendwa wa kunifariji
Nikalia Mungu wangu mbona umeniacha
Ona umeacha fedheha katika maisha yangu
Mungu wangu akasema niko Baba mwenye upendo
Maana mimi naitwa Baba kwa wasio na Baba
Maana mimi ninaitwa mume kwa wasio na mume . .
Wewe ni Baba mwema kwangu, wewe ni Baba
Wewe ni Baba mwema kwangu, wewe ni Baba
Uhimidiwe Mungu wangu, wewe ni Baba ah
Uhimidiwe Mungu wangu, wewe ni Baba ah . .
Wewe ni Baba wa watu wote
Naomba tazama watu wako
Ni wengi wanalia wanakuhitaji Baba
Ni wengi wanajuta wanakuhitaji Yesu
Tazama wengi ni wajane
Tazama wengi ni yatima
Tazama wengi ni wagonjwa
Tazama wengi wametengwa . .
Wengine uchumi umekuwa ni jangwa kwao
Wengine utasa umekuwa fedheha kwao
Watazame Baba aaah . .
Wewe ni Baba mwema kwangu, wewe ni Baba
Wewe ni Baba mwema kwangu, wewe ni Baba
Uhimidiwe Mungu wangu, wewe ni Baba ah
Uhimidiwe Mungu wangu, wewe ni Baba ah