Chorus / Description :
Nimesogea Mtini pako,
Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako
Nasikia kuitwa na sauti yako
Nikasafiwe kwa damu, Ya kwangikwa kwako.
Ni mnyonge kweli,Umenipa nguvu,
Ulivyonisafi taka, Ni utimilivu.
Nasikia kuitwa na sauti yako
Nikasafiwe kwa damu, Ya kwangikwa kwako.
Nimesogea Mtini pako,
Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako
Ni mnyonge kweli,Umenipa nguvu,
Ulivyonisafi taka, Ni utimilivu.
Nimesogea Mtini pako,
Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako
Yesu hunijuvya; Mapenzi, imani;
Tumai, amani, radhi, Hapa na Mbinguni.
Nimesogea Mtini pako,
Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako
Huipa imara, Kazi yake, ndani:
Huongezeka neema, Ashindwe Shetani.
Nimesogea Mtini pako,
Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako
Huishuhudia, Myoyo ya imani
Ya kuzipata ahadi, Wakimuamini.
Nimesogea Mtini pako,
Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako
Napata wokovu, Wema na neema;
kwako Bwana nina nguvu, Na haki daima
Nimesogea Mtini pako,
Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako