Chorus / Description :
Ebenezer
Nani kama wewe
nainama mbele zako Wewe ni Mungu
Moyoni mwangu Yahweh nashukuru sana
Kwa wema wako na fadhili zako kwangu za milele
Umekuwa mwema Imanueli, mwaminifu
Wewe ndiwe pumzi ya imani yangu nakuabudu

Matendo yako maishani mwangu ya tisha Jehovah
Natamani nifanane nawe Messiah Siku zote
Usiye badilika na wakati Elohim u mwema
Ebenezer nani kama wewe nainama mbele zako Wewe ni Mungu

Natamani nifanane nawe usiyebadilika
Uaminifu wako Adonai wa milele na milele,
Toka utotoni mwangu umekuwa mwema sana
Umbali umenileta Yahweh hakuna mwingine kama wewe
Ebenezer nani kama wewe nainama mbele zako Wewe ni Mungu
Ebenezer nani kama wewe nainama mbele zako Wewe ni Mungu
Kwa nehema yako Adonai, umeihifadhi roho yangu
Wengi tulizaliwa nao na wengi sasa wamefariki
Wengine hawakujui Yahweh Mungu mwenye enzi na uzima,
Lakini kwa nehema yako Shamaah umenipa uhai niishi
Ebenezer nani kama wewe nainama mbele zako Wewe ni Mungu
Ebenezer nani kama wewe nainama mbele zako Wewe ni Mungu
Wewe uliye nena na Samweli, hutamdharau mwanadamu,
usiye tazama maumbile, yake wewe Mungu wa haki,
Umbali umenileta Yahweh, Ebeneezer wewe ndiye Mungu,
Mungu mwenye enzi na uzima, uinuliwe milele yote.
Ebenezer nani kama wewe nainama mbele zako Wewe ni Mungu
Ebenezer nani kama wewe nainama mbele zako Wewe ni Mungu
Umekuwa mwema Imanueli, mwaminifu
Wewe ndiwe pumzi ya imani yangu nakuabudu
Umekuwa mwema Imanueli, mwaminifu
Wewe ndiwe pumzi ya imani yangu nakuabudu
Ebenezer means The Stone of Help