Chorus / Description :
Shujaa wa msalaba, umeinuliwa juu
Wacha nikwabudu ewe Mungu wangu
Nainua macho yangu
Nitazame mbinguni
Moyo Wangu unasema niwe Mungu wangu
Kilindi cha moyo Wangu kimefurika neno lako
Wacha nikwabudu ewe Mungu wangu
kwenye kiti cha rehema, kumejawa utukufu wako
Wacha nikwabudu ewe Mungu wangu
kileleni pa msalaba, kumeandikwa jina lako
Simba wa wayahudi ndiwe Mungu waangu
Shujaa wa msalaba, umeinuliwa juu.
Wacha nikwabudu ewe Mungu wangu
Shujaa wa msalaba, umeinuliwa juu.
Wacha nikwabudu ewe Mungu wangu
Wingu la uwepo wako, limeshuka kwa watu wako
Utukufu una wewe ewe Mungu wangu
Nguvu zilizo shinda kaburi
zionekane kwa watu wako.
Nani kama wewe ewe Mungu wangu
Makovu na misumari yatangaza utukufu wako Baba
Wacha nikwabudu ewe Mungu wangu
Taji ya miba na misumari
Yatangaza uwezo wako
Mfalme wa wafalme ndiwe Mungu wangu
Shujaa wa msalaba, umeinuliwa juu
Wacha nikwabudu ewe Mungu wangu
Siku ya msiba wangu
Nitalitaja jina lako
Bwana wa Mabwana ndiwe Mungu wangu
Sitanyamaza mchana sitakaa kimya usiku
Wacha nikusifu ewe Mungu wangu
Nguvu na uweza wako ziko mikononi mwako
Nani kama wewe ewe Mungu wangu
Ulipewa jina jipya lipitalo majina yote
Bwana wa mabwana ewe Mungu wangu
Shujaa wa msalaba, umeinuliwa juu
Wacha nikwabudu ewe Mungu wangu
Shujaa wa msalaba, umeinuliwa juu
Wacha nikwabudu ewe Mungu wangu
Shujaa wa msalaba, umeinuliwa juu
Wacha nikwabudu ewe Mungu wangu