Chorus / Description :
Siku kuu Siku kuu
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu,
Hukesha na kuomba tu,
Ananiongoza miguu,
Suku kuu Siku kuu
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.
Ni siku kuu siku ile,
Ya kumkiri Mwokozi!
Moyo umejaa tele,
Kunyamaza hauwezi.
Siku kuu, Siku kuu,
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.
Hukesha na kuomba tu,
Ananiongoza miguu.
Suku kuu, Siku kuu,
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.
Tumekwisha kupatana,
Mimi wake,Yeye wangu,
Na sasa nitamwandama,
Nikiri neno la Mungu.
Siku kuu, Siku kuu,
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.
Hukesha na kuomba tu,
Ananiongoza miguu.
Suku kuu, Siku kuu,
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.
Moyo tulia kwa Bwana,
Kiini cha raha yako,
Huna njia mbili tena,
Yesu ndiye njia yako.
Siku kuu, Siku kuu,
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.
Hukesha na kuomba tu,
Ananiongoza miguu.
Suku kuu, Siku kuu,
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.
Nadhiri yangu ya mbele,
Nitaiweka daima,
Hata ije siku ile,
Ya kwonana kwa salama.
Siku kuu, Siku kuu,
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.
Hukesha na kuomba tu,
Ananiongoza miguu.
Suku kuu, Siku kuu,
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.