Chorus / Description :
Mke si kidude cha kujaribu miguu yako, Mume si kipasa sauti cha kupigia kelele
Mpendaneni, msichokozane, amani ya Bwana iwe ndani yenu
Ndoa ni mpango takatifu tangu mwanzo,
ujumbe njema utokao kwa Baba,
yahitajika hekima kuitunza
hadi kifo kiwatenganishe.
Chorus
Mke si kidude cha kujaribu miguu yako,
Mume si kipasa sauti cha kupigia kelele
Mpendaneni, msichokozane,
amani ya Bwana iwe ndani yenu.
2. Kazi kwenu sasa maishani mwenu,
mdumu milele kwenye upendo wa Yesu,
ni Mungu pekee aweza kuwalinda na kutatua
mashaka yenu ya Maisha.
Bridge
Muwe mfano bora kwa watoto wenu,
waonyeshe njia ile ya uzima ya wokovu,
Nanyi watoto wote watiini wazazi wenu,
mibaraka yake Mungu 'tawakirimia.