William Yalima - Hata Hili Linapita

Chorus / Description : Hata hili linapita
Hata hili lina mwisho
Hata hili linapita
Hata hili lina mwisho

Hata Hili Linapita Lyrics

Hata hili linapita 
Hata hili lina mwisho 
Hata hili linapita 
Hata hili lina mwisho 

Ni kweli napitia kipindi kigumu 
Moyo wangu unauma 
Nijaribu lililosima mbele zako kizito 
Moyo unafadhaika 
Lakini namwimini Mungu atanivusha tu 
Wakati mwingine nilikumbana na hatari 
Ya kugharimu uhai wangu 
Mungu hakuniacha, MUngu alinibeba 
Hata hili linapita, Hata hili lina ukomo wake 
Kila jaribu linalokuja mbele yangu 
Bibilia linasema lina mlango wa kutokea 
Waswahili wanasema hakuna mrefu lisilokuwa na mwisho 
Hata hili lina mwisho 

Majaribu hayana budi kuyavumilia 
Nitavumilia oh sitawaza uovu 
Manabii walijaribiwa 
mitume wengine kufa kwa ajili ya kazi ya Mungu 
Nami pia sitavunjika moyo 

Vumilia vumilia vumilia jipe moyo 
Vumilia vumilia hatimaye utashinda 

Vikwazo vingi na vitisho mbele yako 
Usiogope usiogope 
Ndoa yako japo kiasi hicho 
Usiogope jibu lipo leo 
Huduma japo pigwa vita hivyo 
Usiogope jua yupo mtetezi 
Ukimwona nyani mzee 
Jua kakwepa mishale mingi 
Usiogope yupo mtetezi 
Usiogope vita ni vya Bwana 
Usiogope vita ni vya Bwana 

Sitaogopa sitaogopa 
Mungu yuko nami 
Sitaogopa sitaogopa 
Sitaogopa atanishindia 

Sitaogopa sitaogopa 
Mungu yuko nami 
Sitaogopa sitaogopa 
Sitaogopa atanishindia 

Hata hili linapita 
Hata hili lina mwisho 
Hata hili linapita 
Hata hili lina mwisho 

Hata Hili Linapita Video

  • Song: Hata Hili Linapita
  • Artist(s): William Yalima


Share: