Uko Wapi

By William Yalima

Lyrics

Uko wapi eh Mungu wangu  

Uko wapi njoo uniokoe


Mawimbi yanataka kuniangamiza 

Misukosuko yaniandama 

Dhoruba na majaribu havikomi kwangu 

Uko wapi fanya hima niokoe 


Uko wapi eh Bwana 

Uko wapi mbona ni kama umeniacha

Usifiche uso wako eh Bwana 

Usifiche uso nipone kwa rehema 

Mwili huu wa nyama 

unachoka pekee yangu sitaweza


Nimegumbikwa wimbi la huzuni na mawazo 

Amani kwangu ni kama ndoto 

Ole wangu nikifurahi siku moja 

Siku sita nitalia wiki ipite 

Mangumu yangu nikisimulia kwa ndugu zangu 

Waniambia utajijua na Mungu wako 

Nikielezea magumu yangu kwa wapendwa 

Waniambia tumechoka kukufariji 

Wakati mwingine natamani heri nife

Kuliko kuishi ninyanyasike hivi 


Uko wapi eh Mungu wa Elijah 

Uko wapi eh Mungu wa Ibrahimu 

Uko wapi eh Mungu wa isaka 

Elshadai fanya hima uniokoe 

Uko wapi eh Bwana  

Uko wapi mbona ni kama umeniacha 

Usifiche uso wako eh Bwana 

Usifiche uso nipone kwa rehema 

Mwili huu wa nyama 

Unachoka pekee yangu sitaweza


Nina neno juu yako eh mpendwa 

Usilie kwa mangumu uliyonayo 

Usitazame jaribu ulilonalo 

Inua macho msalabani umtazame yesu 

Japo ndugu wakikutenga na kukuacha 

Yesu atakukumbatia majaribu ipo siku yatakoma 

Utasahau shida zote ulizopata 

William R Yilima - Uko Wapi Mungu