Ninajulikana Mbinguni

by Martha Mwaipaja

Ninajulikana mbinguni, ninaheshimiwa mbinguni

Nimehesabiwa na Yesu mwenyewe 

Ananitsha milele 

Ninajulikana kwa Baba, ninaendelea kwa Yesu

Nimehesabiwa mbinguni juu 

Amenipenda mimi mwokozi

Sijajiweka mwenyewe mimi mwenzio 

Nimewekwa na Mungu 

Sijawai jitambulisha mwenyewe 

Nimetambulishwa na Baba 

Walisemezana tusimtambulishe huyu 

Nimetambulishwa mbinguni ii

Wakasema tusimchague, nimechaguliwa mbinguni 

Wakasema tusimkubali, nimekubaliwa na Baba 

Nimewekwa na Mungu mwenyewe, najulikana mbinguni 

Hahaa najulikana mbingu

Ninajulikana mbinguni, ninaendelea na Yesu 

Ninajulikana mbinguni, ninaendelea na Yesu 

Ninajulikana mbinguni, ninaendelea na Yesu 

Ninajulikana mbinguni, ninaendelea na Yesu 

Unajulikana mbinguni rafiki, mbingu inakujua 

Wametangaziana wasikusaidie, umesaidiwa na Mungu 

Wameambizana wasikutendee mema, umetendewa na Baba 

Wamesema wasikufute kwenye ukoo wao, umeandikiswa mbinguni 

Wamekataa kukutambulisha, unatambulishwa na Mungu 

Walisema hawatakujibu kabisa umeponywa na Mungu 

Wamekataa kukubeba, utabebwa na Yahweh 

Hujui vile nimependwa na Mungu 

Ninajulikana mbinguni, ninaendelea na Yesu

Ninajulikana mbinguni, ninaendelea na Yesu

Ninajulikana mbinguni, ninaendelea na Yesu

Ninajulikana mbinguni, ninaendelea na Yesu

Share