1 Petro Mlango 3 1st Peter

1 Petro 3:1 1stPeter 3:1

Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;

1 Petro 3:2 1stPeter 3:2

wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.

1 Petro 3:3 1stPeter 3:3

Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;

1 Petro 3:4 1stPeter 3:4

bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.

1 Petro 3:5 1stPeter 3:5

Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.

1 Petro 3:6 1stPeter 3:6

Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote.

1 Petro 3:7 1stPeter 3:7

Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

1 Petro 3:8 1stPeter 3:8

Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;

1 Petro 3:9 1stPeter 3:9

watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.

1 Petro 3:10 1stPeter 3:10

Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila.

1 Petro 3:11 1stPeter 3:11

Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana.

1 Petro 3:12 1stPeter 3:12

Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya.

1 Petro 3:13 1stPeter 3:13

Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?

1 Petro 3:14 1stPeter 3:14

Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu.

1 Petro 3:15 1stPeter 3:15

Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.

1 Petro 3:16 1stPeter 3:16

Nanyi mwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.

1 Petro 3:17 1stPeter 3:17

Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya.

1 Petro 3:18 1stPeter 3:18

Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa,

1 Petro 3:19 1stPeter 3:19

ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri;

1 Petro 3:20 1stPeter 3:20

watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.

1 Petro 3:21 1stPeter 3:21

Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.

1 Petro 3:22 1stPeter 3:22

Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake.