Wakolosai Mlango 3 Colossians

Wakolosai 3:1 Colossians 3:1

Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu.

Wakolosai 3:2 Colossians 3:2

Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.

Wakolosai 3:3 Colossians 3:3

Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.

Wakolosai 3:4 Colossians 3:4

Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu.

Wakolosai 3:5 Colossians 3:5

Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;

Wakolosai 3:6 Colossians 3:6

kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu.

Wakolosai 3:7 Colossians 3:7

Katika hayo ninyi nanyi mlitembea zamani, mlipoishi katika hayo.

Wakolosai 3:8 Colossians 3:8

Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu.

Wakolosai 3:9 Colossians 3:9

Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake;

Wakolosai 3:10 Colossians 3:10

mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba.

Wakolosai 3:11 Colossians 3:11

Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala mwungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote.

Wakolosai 3:12 Colossians 3:12

Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,

Wakolosai 3:13 Colossians 3:13

mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.

Wakolosai 3:14 Colossians 3:14

Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.

Wakolosai 3:15 Colossians 3:15

Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.

Wakolosai 3:16 Colossians 3:16

Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

Wakolosai 3:17 Colossians 3:17

Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.

Wakolosai 3:18 Colossians 3:18

Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.

Wakolosai 3:19 Colossians 3:19

Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.

Wakolosai 3:20 Colossians 3:20

Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana.

Wakolosai 3:21 Colossians 3:21

Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.

Wakolosai 3:22 Colossians 3:22

Ninyi watumwa, watiini hao ambao kwa mwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wanadamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimcha Bwana.

Wakolosai 3:23 Colossians 3:23

Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu,

Wakolosai 3:24 Colossians 3:24

mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.

Wakolosai 3:25 Colossians 3:25

Maana adhulumuye atapata mapato ya udhalimu wake, wala hakuna upendeleo.