Wakolosai Mlango 1 Colossians

Wakolosai 1:1 Colossians 1:1

Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo, ndugu yetu,

Wakolosai 1:2 Colossians 1:2

kwa ndugu watakatifu, waaminifu katika Kristo, walioko Kolosai. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu.

Wakolosai 1:3 Colossians 1:3

Twamshukuru Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, siku zote tukiwaombea;

Wakolosai 1:4 Colossians 1:4

tangu tuliposikia habari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote;

Wakolosai 1:5 Colossians 1:5

kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni; ambalo habari zake mlizisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili;

Wakolosai 1:6 Colossians 1:6

iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, na kuzaa matunda na kukua, kama inavyokua kwenu pia, tangu siku mlipoisikia mkaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli;

Wakolosai 1:7 Colossians 1:7

kama mlivyofundishwa na Epafra, mjoli wetu mpenzi, aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu;

Wakolosai 1:8 Colossians 1:8

naye alitueleza upendo wenu katika Roho.

Wakolosai 1:9 Colossians 1:9

Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;

Wakolosai 1:10 Colossians 1:10

mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;

Wakolosai 1:11 Colossians 1:11

mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;

Wakolosai 1:12 Colossians 1:12

mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru.

Wakolosai 1:13 Colossians 1:13

Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;

Wakolosai 1:14 Colossians 1:14

ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;

Wakolosai 1:15 Colossians 1:15

naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.

Wakolosai 1:16 Colossians 1:16

Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.

Wakolosai 1:17 Colossians 1:17

Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.

Wakolosai 1:18 Colossians 1:18

Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.

Wakolosai 1:19 Colossians 1:19

Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae;

Wakolosai 1:20 Colossians 1:20

na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.

Wakolosai 1:21 Colossians 1:21

Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa;

Wakolosai 1:22 Colossians 1:22

katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama;

Wakolosai 1:23 Colossians 1:23

mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake.

Wakolosai 1:24 Colossians 1:24

Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake;

Wakolosai 1:25 Colossians 1:25

ambalo nimefanywa mhudumu wake, sawasawa na uwakili wa Mungu, niliopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la Mungu;

Wakolosai 1:26 Colossians 1:26

siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake;

Wakolosai 1:27 Colossians 1:27

ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu

Wakolosai 1:28 Colossians 1:28

ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo.

Wakolosai 1:29 Colossians 1:29

Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu.